ATCL Yarejesha Safari za Ndege India

SAFARI za ndege kutoka Tanzania kwenda Mumbai- India zimerejea kuanzia leo Jumapili Agosti 29, 2021 baada ya kusitishwa mwezi Mei mwaka huu.
Mwezi Mei 2021, Serikali ilitangaza kusitisha safari za ndege kutoka Tanzania kwenda India ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na maambukizi ya Uviko-19.
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amewaeleza waandishi wa habari jana Jumamosi Agosti 28 jijini Dodoma kwamba safari hizo zitaanza leo huku Serikali ikiendelea kujipanga kufungua maeneo mengine.
India ilikuwa inakabiliwa na janga kubwa la virusi vya corona, hospitali zilikuwa zimelemewa wagonjwa wengi na ripoti za watu kufariki mitaani .

