Benki Ya Stanbic Yatoa Misaada Ya Vifaa Tiba Mkoani Mwanza

Mwanza Novemba 27,2025. Benki ya Stanbic imekabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda, mashuka na viti mwendo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 19 kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri ya jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mwanza, Geofrey Makondo amesema “Kama wadau wa maendeleo ya sekta ya Afya wamewiwa kukabidhi vifaa hivyo na wamekuwa na utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii. Mpango huu ni sehemu endelevu wa uwajibikaji wa kijamii wa Benki ya Stanbic unaolenga kurudisha fadhila kwa jamii, sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya kukua pamoja tangu benki hiyo ianze kutoa huduma nchini Tanzania”. alisema Makondo
“Tunatambua mchango mkubwa wa sekta ya afya katika ustawi wa jamii. Kupitia msaada huu, tunalenga kusaidia hospitali na vituo vya Afya mkoani Mwanza ili vitoe huduma bora zaidi kwa wagonjwa na kuongeza ufanisi wa watoa huduma.

Naye Katibu Tawala mkoa wa Mwanza, Erikana Balandya akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda katika hafla hiyo amesema sekta ya Afya ni muhimu hivyo kutolewa kwa vifaa tiba hivyo kutaongeza chachu ya utoaji huduma.
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, Daktari Kwandu Mashuda akimwakilisha mganga mkuu wa mkoa huo Jesca Lebba amewashukuru wadau hao wa sekta ya Afya huku kaimu mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Zena Kapama akiwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia.
Bank ya Stanbic Bank Tawi la Mwanza imekabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda, mashuka na viti mwendo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 19 kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri ya jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

