The House of Favourite Newspapers

Boris Johnson Aaga na Kukabidhi Mikoba kwa Waziri Mkuu Mpya Bi. Liz Truss

0
Borris Johnson na Liz Truss

LEO septemba 6 waziri mkuu mpya wa uingereza atachukua madaraka rasmi kama Waziri mkuu

Liz Truss anachukua nafasi ya Boris Johnson kama Waziri Mkuu wa Uingereza siku ya leo Jumanne akisafiri kumwona Malkia Elizabeth huko Scotland kabla ya kuteua mawaziri wa vyeo vya juu katika baraza lake la mawaziri ili kushughulikia mzozo wa kiuchumi na kuunganisha chama chake kilichogawanyika.

 

Truss alimshinda mpinzani wake Rishi Sunak katika upigaji kura wa wanachama wa uwongozi wa chama cha Conservative na kuahidi kupunguza kodi na kuwasaidia watu kulipa bili zao za nishati wakati Uingereza inakabiliwa na shida ya nishati inayoongezeka.

Waziri mkuu mpya Bi.Liz Truss

“Asante kwa kuweka Imani yako kwangu kukuongoza na kujitoa kwa ajili ya nchi yetu nzuri, Truss alisema. Nitachukua hatua shupavu kutuvusha sote katika nyakati hizi ngumu, kukuza uchumi wetu na kuibua uwezo wa Uingereza”.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply