Chrome Ilivyowasha Moto Uzinduzi Tanzania, Chapa Mpya Inayosherehekea Vijana Wapambanaji Nchini
Dar es Salaam. Vijana wa Kitanzania na hustlers kutoka sehemu mbalimbali walikusanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe – Dar es Salaam (August 30, 2025) kushuhudia uzinduzi wa kifahari wa Chrome, chapa mpya kutoka Serengeti Breweries Limited (SBL). Kupitia ladha zake mbili za kipekee – Gin na Vodka – Chrome siyo tu kinywaji; ni chapa iliyobuniwa kuinua, kuwawezesha na kusherehekea mamilioni ya Watanzania wanaopambana kila siku kufanikisha ndoto zao.
Uzinduzi huo ulikuwa na shamrashamra za kipekee na ubunifu, uliovutia maelfu ya vijana walioungana kusherehekea mafanikio yao – makubwa na madogo. Kuanzia waendesha bodaboda, vinyozi, wauza nguo, wasanii mpaka wajasiriamali, Chrome imejikita kwa kila anayejituma, anayevuka mipaka na kuamini kuwa siku moja juhudi zake zitazaa matunda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gwamaka Mwankusye, Meneja wa Habari wa SBL, alisisitiza filosofia ya Chrome: “Chrome siyo tu kinywaji. Ni harakati inayoheshimu juhudi, ari na mafanikio ya vijana wa Kitanzania. Iwe ni hatua ndogo au mafanikio makubwa ya kubadilisha maisha, Chrome ipo kusherehekea kila hatua ya safari hiyo.”
Tukio hilo lilienda mbali zaidi ya burudani – liliwapa wajasiriamali wa ndani fursa ya kuonyesha kazi zao na kuunganishwa na wateja wapya. Mbunifu wa mitindo Audrey Erasrus na msanii wa tattoo Simba Lameck walikuwa miongoni mwa walionufaika.
“Jukwaa hili limenisaidia sana kama mbunifu. Nimekutana na watu ambao wanaweza kuwa wateja wa muda mrefu,” alisema Audrey.
Simba naye aliongeza: “Kujulikana ni kila kitu katika kazi yetu. Uzinduzi huu ulinipa nafasi ya kuonyesha ubunifu wangu na kupata wateja wapya papo hapo.”
Kwa kuwapa hustlers jukwaa, Chrome ilionyesha dhamira yake ya kuwawezesha wale ambao chapa hii imebuniwa kwa ajili yao – vijana wapambanaji wanaoendelea kuipeleka Tanzania mbele.
Umati ulipagawishwa na performance za nguvu kutoka kwa DJ Joozey, D Voice, Chino Kidd na Dogo Rema, waliowasha moto jukwaani kwa ‘vibe la aina yake! Burudani hizo zilitengeneza mazingira ya kipekee ambapo hustlers walipumzika, kusherehekea safari zao na kufurahia Chrome Gin na Vodka.
Lakini usiku huo haukuwa wa burudani pekee – ulikuwa ni ujumbe. Uliashiria kuwa utamaduni wa hustlers nchini Tanzania una nguvu na ubunifu ndani yake na unastahili kusherehekewa. Chrome sasa imejipambanua kama kinywaji kinachowaunganisha marafiki, familia na jamii kusherehekea mafanikio yaliyopatikana kwa jasho na juhudi zao.
Kwa uzinduzi huu wa mafanikio, Chrome imefungua rasmi safari yake nchini Tanzania. Kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa mingine, chapa hii ina mpango wa kuendelea kuinua na kuwawezesha hustlers kwa kusimulizi zaidi story zao. Iwe ni Mbagala, Mwanza au Arusha, Chrome imejikita kukuza sauti na mafanikio ya vijana wa Kitanzania.
Kadri Serengeti Breweries Limited inavyopanga kuendeleza shughuli za Chrome mtaani, jambo moja ni dhahiri: Chrome siyo tu kinywaji – ni chapa inayoendana na maisha yetu ya kila siku na inayosherehekea juhudi, ustahimilivu na imani kwamba kila ushindi wa hustler unastahili kuthaminiwa.