Bluu Yagusa Maisha Ya Wagonjwa Hospitali Ya Mwananyamala Na Amana

Akizungumza na mwandishi wetu Oktoba 18, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa msaada huo, Mwakilishi wa Bluu, Bw. Hamisi Athumani, amesema kuwa hatua hiyo ni mwanzo wa mpango mkubwa wa taasisi yao kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii.

“Lengo letu ni kuwawezesha kiuchumi Watanzania waliokumbwa na changamoto mbalimbali ili waweze kufanikisha malengo yao, yakiwemo kupata huduma muhimu kama dawa,” amesema Bw. Athumani.
Aidha, amebainisha kuwa msaada huo ni hatua ya awali na kwamba taasisi hiyo imejipanga kufika katika mikoa mingine nchini, hasa ile yenye uhitaji mkubwa zaidi.

“Huu ni mwanzo tu. JAMBO KUBWA LINAKUJA, BLUU INATAWALA. Tumeanza kwa kuwasaidia wagonjwa hapa hospitalini kwa kiwango kidogo, lakini tumejipanga kufanya zaidi,” ameongeza.
Kwa upande wao, baadhi ya wagonjwa waliopokea msaada huo, akiwemo Bi. Renetha Fabiani na Bw. Hemedi Shabani, wameeleza furaha yao na kutoa shukrani kwa taasisi ya Bluu kwa msaada walioupata, huku wakisema kuwa umewasaidia kupata dawa ambazo awali walishindwa kuzimudu kifedha.
Mr.Blue wamewataka Watanzania kusubiri hivi karibuni watajua ni jambo gani kubwa ambalo limekuja, na Watanzania watajua.
