Jux na Huddah Kuna Mtu Anapigwa Tukio, Akumbushwa ya Ben Pol

HUDDAH Monroe; ni mrembo maarufu mitandaoni ambaye inadaiwa ni mdangaji wa kimataifa wa nchini Kenya akijihusisha na ‘biashara zake’.
Sasa; wikiendi iliyopita Huddah ametua Bongo na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni staa wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Juma Jux.
Taarifa ikufikie kwamba, Huddah hakupokelewa hivihivi; amepokelewa kwa mabusu mazito kutoka kwa Jux kuanzia uwanja wa ndege, nyumbani kwa Jux na wakatoka kwenda klabu usiku.
Ingawa Huddah amekuja Bongo kikazi zaidi, lakini ukweli ni kwamba huwa anampenda mno Jux hivyo Jux ndiye atakuwa mwenyeji wake Tanzania kwa hizi siku chache ambazo atakuwa Bongo.
Dalili ya kutoka kimapenzi zimeanza kuonekana ambapo katika moja ya video zao wanaonekana wakipigana mabusu ya hatari huku wakiwa na hisia nzito mno.
Kwa maana hiyo lolote linaweza kutokea au limeshatokea kati yao.
Lakini ikitokea Jux akatoka kimapenzi na Huddah inabidi awe makini mno kwa sababu atapigwa tukio muda wowote.

Jux anakumbushwa kwamba wanawake wa Kenya kwa sasa wanajulikana kinagaubaga; mfano ni Ben Pol na Anerlisa.
Wapo wanaosema Huddah atamsababishia umaskini Jux na The African Boy itasahaulika kama ataendekeza mapenzi na Huddah.
Ukipitia mitandao ya udaku ya Kenya, inamtaja Huddah kwamba siyo mwanamke wa Kuishi naye.
Pia ukipitia tu posti za Huddah kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii utaona posti zake ni nusu Utupu, sasa hapo Jux ajichanganye aone jua litakavyomuwakia!
Cc; @sifaelpaul