The House of Favourite Newspapers
gunners X

Niffer na Mika Chavala Warudishwa Gerezani, Kesi yao Kutajwa Desemba 3

0
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ameondoa mashtaka dhidi ya washtakiwa 20 waliokuwa wakikabiliwa na shtaka la uhaini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, huku mtuhumkwa  mfanyabiashara Jeniffer Jovin ‘Niffer’ na Mika Chavala wakiwa hawapo miongoni mwao na kesi yao imepangwa kutajwa Desemba 3, 2025.
Hatua hiyo imeelezwa leo mahakamani na Wakili wa Serikali, Titus Aaron, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.
“Shauri lilipangwa kwa ajili ya maamuzi madogo, ila kabla ya mahakama kutoa maamuzi hayo, Upande wa Jamhuri tuna ombi. Mkurugenzi wa Mashtaka ameonelea kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa wote isipokuwa Jeniffer na Mika Chavala,” alisema wakili Aaron.
Uamuzi huu umejitokeza siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuitaka Ofisi ya DPP kutathmini upya mashtaka ya uhaini yaliyokuwa yakiwakabili baadhi ya watuhumiwa, akielekeza kuangalia uwezekano wa kuwaondolea mashtaka hayo pale inapostahili.
Hatua ya leo imekuwa miongoni mwa utekelezaji wa maelekezo hayo, ambapo tayari baadhi ya watuhumiwa wameanza kuachiwa huru toka juzi.
Leave A Reply