The House of Favourite Newspapers

Pakistan Yapata Waziri Mkuu Mpya, Anaenda Kuchukua Nafasi ya Yule Waliyemtimua

0
                          Waziri Mkuu Mpya mteule wa Pakistan Shehbaz Sharif

BUNGE la Pakistan leo limepiga kura kumchagua Waziri Mkuu mpya wan chi hiyo kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mpya wan chi hiyo Imran Khan baada ya kupigiwa kura za kutokuwa na Imani naye.

 

Shehbaz Sharif ndiye Waziri Mkuu Mpya aliyechaguliwa na Bunge la Pakistan, Shehbaz

 

Kuelekea uchaguzi huo baadhi ya wabunge kutoka Chama cha Khan waligomea uchaguzi wa Shehbaz, ni mdogo wa aliywahi kuwa Waziri Mkuu mara tatu wan chi hiyo Nawaz Sharif.

 

Sherehe za kuapishwa zinatarajiwa kufanyika jioni ya leo jumatatu.

 

Taarifa zinasema kuwa uchaguzi ulikuwa chini ya ulinzi wa hali ya juu huku barabara zote zinazoelekea Bungeni zikifungwa.

                                     Sherehe za kuapishwa kwake zinafanyika jioni ya leo jijini Islamabad

Sharif ambaye ndiye aliyeongoza harakati za kumng’oa madarakani Khan ameahidi kuwa serikali yake itaimarisha uchumi na si kulipiza visasi kwa wapinzani wake wa kisiasa.

 

Sharif mwenye umri wa miaka 70 amezaliwa katika familia ya kitajiri yenye uwekezaji mkubwa wa viwanda ambao wamekuwa watawala wa kubwa katika siasa za nchini Pakistan.

 

Alichaguliwa kujiunga na Bunge mwaka 2018 na akaongoza chama cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) baada ya kaka yake kufungiwa maisha kutojihusisha na siasa baada ya kukumbwa na kashfa ya rushwa.

 

Leave A Reply