Putin Aruhusu Waangalizi wa Umoja wa Mataifa Kutembelea Kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia

RAIS wa Urusi Vladimir Putin amekubali waangalizi na wakaguzi kutoka Umoja wa Mataifa kutembelea eneo la kinu cha Nyuklia la Zaporizhzhia la nchini Ukraine linaloshikiliwa na majeshi ya Urusi.
Taarifa kutoka Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imebainisha kuwa Rais Putin alishauri Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (1AEA) kufanya ziara kwa kupitia njia ya nchini Urusi na kusisitiza kuwa mapigano kufanyika katika maeneo yale yatasababisha maafa zaidi.

Licha ya pendekezo hilo kutopokelewa na waangalizi hao wa Umoja wa Mataifa ndipo Putin alipoamua kuwaruhusu Kwenda katika kinu hicho kwa kupitia njia ya Ukraine.
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyataka majeshi ya Urusi yanayoshikilia kiwanda hicho cha utengenezaji wa vinu vya nyuklia kutotenganisha nishati na mkongo wa umeme wa Taifa ili wananchi wasiathirike kwa kukosa huduma ya nishati ya umeme.