The House of Favourite Newspapers

Rais Dkt. Mwinyi Akutana na Kufanya Mazungumzo na Jenerali Mabeyo

0
Rais Mwinyi akifanya mazungumzo na Jenerali Mabeyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kuja kumuaga, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.

 

Jenerali Mabeyo yupo katika ziara yake maalum ya kuaga kwa ajili ya kustaafu.

 

Rais Mwinyi alifanya kazi na Jenerali Mabeyo kwa kipindi kirefu wakati huo ambao Rais Mwinyi akiwa Waziri katika Wizara ya Ulinzi.

Jenerali Mabeyo yupo katika ziara maalum ya kuaga kuelekea Kustaafu

Katika mazungumzo yao Rais Mwinyi amemshukuru Jenerali Mabeyo kwa ushirikiano aliompatia wakati wakifanya kazi pamoja katika Wizara ya Ulinzi lakini pia amempongeza kwa utendaji kazi wake kwa kulitumikia Taifa lake la Tanzania kwa juhudi na Uadilifu wa hali ya juu.

 

Mwisho Dkt. Mwinyi amemtakia kheri na maisha marefu Jenerali Mabeyo katika maisha yake mapya baada ya kustaafu.

Leave A Reply