The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amfuta Kazi Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa MSD, Afanya Uteuzi Mwingine

0
Rais Samia Suluhu Hassan yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemfuta kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).

 

Kufutwa kazi kwa Mwenyekiti huyo kumetokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini Bohari hiyo ilishikilia zaidi ya shilingi bilioni 14 za Hospitali kwa mwaka mzima bila kupeleka dawa na vifaa tiba katika hospitali mbalimbali.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus moja kwa moja kutoka Washington DC nchini Marekani imesema Rais Samia amemteua Afisa Mwandamizi wa Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC), Rosemary Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa.

 

Pia Rais Samia amemteua Kiongozi Mkuu wa Mradi wa Usaid Global Health Supply Chain Technical Assistance, Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)

Leave A Reply