The House of Favourite Newspapers

Serikali Kuunga Mkono Uwekezaji Mazao ya Bustani

0

SERIKALI  ya awamu ya tano imesisitiza kuwa itaendelea kuunga mkono uwekezaji  katika  mazao ya bustani ili kuikuza sekta hiyo ambayo ina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi nchini na kuchochea ajira.

 

Hayo yamesemwa leo, Desemba 5, 2020, na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akifungua Kongamano la Kikanda la Biashara la Uwekezaji katika Tasnia ya Mazao ya Bustani lililofanyika kwenye Hoteli ya The Kilimanjaro Hyatt Regency, jijiji Dar es Salaam.

 

Majaliwa ametoa uhakikisho huo na kuongeza kwamba mazao ya bustani kama mbogamboga na matunda yamekuwa na mchango mkubwa katika kudhibiti ugonjwa wa COVID- 19.

 

 

Mbali na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, amefafanua, tasnia hiyo inasaidia kujenga taifa lenye watu wenye afya nzuri, nguvu na uwezo wa kufanya kazi, pia ni chanzo kikuu cha lishe na afya bora kwa Watanzania kutokana na virutubisho vingi  kwa ulaji wa mbogamboga, matunda na viungo.

Leave A Reply