The House of Favourite Newspapers
gunners X

Serikali ya Tanzania Yaingia Ubia na Aga Khan Kukabiliana na Ugonjwa wa Saratani

0
             Waziri Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari

WAZIRI wa Afya Ummy awataka watanzania kuacha dhana ya kwenda kwa waganga wa kienyeji na badala yake waende hospitali kupima afya zao na kupewa matibabu.

 

Waziri Ummy ameyasema hayo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha matibabu ya saratani  kwa mradi wa ubia kwa ajili ya kuimarisha huduma za matibabu ya saratani nchini Tanzania kati ya Serikali na Taasisi ya Agakhan.

 

Amesema kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa saratani karibu 42,000 kwa mwaka, na katika wagonjwa 42,000 asilimia 68 ya wagonjwa hao hufariki kila mwaka kutokana na kuugua saratani.

 

Kwa mujibu wa waziri Ummy mradi huu utasaidia kuwafikia watanzania wengi kwa kupima pamoja na kuwapatia matibabu ya ugonjwa wa saratani na kituo hicho kinataraji kuhudumia Zaidi ya wagonjwa 120 kwa siku.

 

Amesema kwa sasa Hospitali ya saratani ya Ocean Road inahudumia wagonjwa kati ya 800 hadi 900 kwa siku hivyo kufunguliwa kwa kituo hicho kutasaidia kuipunguzia mzigo Hospitali ya Ocean Road.

 

Kwa upande mwingine Waziri Ummy ametoa rai kwa watanzania kuwa na utaratibu wa kupima au kuchunguza afya zao mapema ikiwemo ugonjwa wa Saratani.

 

Amedai katika kila wagonjwa 80 kati ya 100 wanaohudhuria katika hospitali ya saratani ya Ocean Road wanakuwa wamefikia hatu ya mwisho kabisa ambayo ni ya hatari na wengi wao hupoteza maisha.

Leave A Reply