Simba Yatuma Salamu za Pole kwa Watani Wao wa Jadi Yanga Kufuatia Kifo cha Shabiki
KLABU ya soka ya Simba imetuma salamu za pole kwa Uongozi wa Klabu ya yanga kufuatia ajali iliyosababisha kifo cha shabiki mmoja wa klabu hiyo anayefahamika kama Dada Hadija.

Katika taarifa hiyo klabu ya Simba pia imewatakia kila lakheri majeruhi na kuwaombea wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao.