Soko la Vetenari, TAZARA Lateketea Kwa Moto Usiku wa Manane

SOKO la Vetenari lililopo maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto ulioanza majira ya saa nane za usiku wa kuamkia Mei 30, 2022.
Kamanda wa zimamoto Mkoa wa Zimamoto Temeke, Michael Bachubira amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na jitihada za kuuzima moto huo ili usiathiri maeneo mengine zimefanyika.

Ingawa hadi sasa chanzo cha ajali hiyo ya moto hakijafahamika.
Kumekuwa na muendelezo wa matukio ya Masoko kuungua moto jijini Dar es Salaam ambapo kwa mwaka huu pekee masoko ya Mbagala na Karume yameungua mara mbili.