Wanawake Wajasiliamali Wanufaika Na Kampeni Ya “Jambo Kubwa Linakuja, Bluu Inatawala”

Akizungumza na waandishi watu leo Oktoba 20, 2025, Dar es Salaam wakati wa kutoa msaada huo, Mwakilishi wa Bluu, Bw. Hamisi Athumani Maarufu kama Mr. Bluu, amesema kuwa hatua hiyo ni mwanzo wa mpango wa taasisi hiyo wa kuwawezesha makundi maalamu ikiwemo wajasiriamali.

“Lengo letu ni kuwawezesha kiuchumi wanawake wajasiriamali wadogo ili waweze kufanikisha malengo yao na kupiga hatua katika maisha yao ya kiuchumi,” amesema Bw. Athumani.
Aidha, amebainisha kuwa msaada huo ni wa mwanzo tu, huku akisisitiza kuwa Bluu imejipanga kuwafikia wananchi wa mikoa mingine yenye uhitaji mkubwa zaidi nchini.
“Huu ni mwanzo tu. JAMBO KUBWA LINAKUJA, BLUU INATAWALA. Tunaendelea kuwasaidia makundi mbalimbali, na si kwa kiwango kidogo. Tumejipanga kufanya zaidi,” ameongeza.
Kwa upande wao, baadhi ya wanawake wajasiriamali waliopokea msaada huo, akiwemo Bi. Lucy Mshambo na Bi. Zainabu Saidi, wameeleza furaha yao na kutoa shukrani kwa taasisi ya Bluu kwa kuwawezesha kupitia msaada huo, huku akisema utawasaidia kukuza mitaji na kuboresha biashara zao.

“Tunashukuru sana kwa msaada huu. Umekuja wakati muafaka na utatupa nguvu mpya ya kuendeleza biashara zetu,” amesema Bi. Mshambo.
