
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora, Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo.
Amechukua hatua hiyo baada ya kukagua mradi huo na kuonesha kutoridhika na gharama za ujenzi wa baadhi ya majengo ikiwemo kibanda cha mlinzi ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 11.

Waziri mkuu amewachukulia watumishi hao hatua hiyo, baada ya kuona majengo yaliyojengwa hapo yamechukua tu gharama za kawaida ikiwemo kibanda cha mlinzi ambacho kwa hali ya kawaida hakistahili gharama kubwa kiasi hicho cha fedha kilichotajwa hapo juu
Hii ni dalili kuwa Fedha iliyoelekezwa katika mradi huo imetumika kinyume na malengo ya mradi huo, hivyo kuna dalili za ubadhilifu wa fedha ambao ulitendwa na wasimamizi hao.
Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.