
YANGA imeshindwa kutamba baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya CRBelouizdad katika mchezo wa Kundi D kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Stade du 5 Juillet Nchini Algeria.
Licha ya kuonesha soka la ushindani muda mwingi wa mchezo huo, Yanga imeshindwa kufunga na kuruhusu lango lake kutikiswa na Abdelraouf Benguit dakika ya 10, Abderrahmane Meziane dakika ya 45 na Lamin Jallow dakika ya 90
Mchezo ujao kwa Yanga itakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kuikaribisha #AlAhly ya Misri, Desemba 2, 2023
