
#ZIROMALARIA: Unaambiwa mbu anayeeneza Malaria hamuogopi baunsa wala mtu yeyote! Usipofuata maelekezo ya jinsi ya kujikinga na Malaria lazima utaambukizwa.
Ili kuwa salama, #Bi-Mdashi ambaye ndiye mhamasishaji wa jamii katika kupambana na ugonjwa wa Malaria, anakukumbusha kuchukua hatua zifuatazo kudhibiti Malaria.
– Lala ndani ya chandarua chenye dawa kila siku ili kujikinga dhidi ya mbu waenezao Malaria.
– Dhibiti mazalia ya mbu kwa kutunza mazingira.
– Nenda kapime kabla ya kutumia dawa za Malaria kwani siyo kila homa ni Malaria.
– Wahi kituo cha huduma za afya afya mara tu unapohisi dalili za Malaria upate tiba sahihi.
– Kamilisha dozi ya dawa mseto la Malaria kulingana na maelekezo ya mtoa huduma ili upone.
#ZiroMalaria Inaanza na Mimi, Nachukua hatua Kuitokomeza.
Tangazo hili linakujia kwa udhamini wa Wizara ya Afya chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria.

