Video: Zlatan Amtwanga Mtu Konde Uwanjani – Video
STAA wa soka Duniani, Zlatan Ibrahimovic jana aliushangaza ulimwengu wa mpira wa miguu baada ya kubadili uwanja wa soka kuwa uwanja wa masumbwi alipomtwanga konde mchezaji mwenzake wa Montreal Impact, Michael Petrasso.
Baada ya kumpiga, Michael alianguka chini na Zlatan naye alijiangusha akionyesha kama amekanyagwa vibaya mguuni kumbe yeye ndiye amemshushia kipigo heavy mchejazi huyo.
Zlatan alifanya kitendo hicho wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Marekani ambapo timu yake ya LA Galaxy ilipokuwa ugenini ikicheza na Montreal Impact kwenye uwanja wa Saputo ambapo galaxy waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Tukio hilo lilifanyika dakika ya 40 ya mchezo huo baada ya mchezaji wa Montreal, Michael Petrasso, kumkanyaga kwenye mguu wake wa kulia ndipo alipochukua maamuzi ya kumpiga kibao hiko. Refa alimtwanga Michael kadi ya njano huku akimlima kadi nyekundu Zlatan ambaye aliwahi kuzichezea Juventus, Barcelona na Manchester United msimu uliopia.


Comments are closed.