Emery: Arsenal itamaliza ndani ya top 4

UNAI Emery ana matumaini kuwa kipigo cha mabao 3-2 walichokipata kutoka kwa Crystal Palace juzi, hakitazima ndoto zao za kumaliza ndani ya nne bora kwenye Premier.
Arsenal walichapwa kichapo hicho kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Emirates, lakini leo Jumatano wana nafasi ya kusawazisha makosa watakapokutana na Wolverhampton ugenini katika mechi hiyo ya Premier.

Katika mchezo wa Jumapili iliyopita, Arsenal ilipoteza nafasi muhimu ya kuingia ndani ya tatu bora lakini kocha Emery amesema: “Ni matokeo mabaya lakini nne bora bado ipo kwenye mikono yetu na haibadilishi kitu kuhusu wapi tutaishia.”
Arsenal inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa katika nafasi ya tano pointi moja nyuma ya Chelsea, lakini ikiwa na mchezo mmoja nyuma ya Chelsea iliyo katika nafasi ya nne.


Comments are closed.