The House of Social Media
gunners X

Serikali: Chini ya Tsh 1,000 Hakuna Tozo – Video

0

Serikali imesema imeamua kutoa punguzo la miamala ya simu kwa 30% kwa watu wanaotuma na kupokea fedha. Kwa wanaotuma kwenda mitandao mingine, makampuni ya simu yamekubali kupunguza tozo kwa 10%. Hizi ni kuanzia Tsh 1,000 kwenda juu, ambapo chini ya Tsh 1,000 hakuna tozo.

 

Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Septemba 4, 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

 

“Serikali imetoa muda wa kati ya tarehe 01 – 07 Septemba, 2021 kwa kampuni hizi za simu kuweka sawa mitambo yao ili punguzo hili lianze. Naomba kusisitiza, tozo hii imewekwa ili kuharakisha utatuzi wa changamoto hizi za wananchi. Kwa sababu tukiendelea kwa kasi iliyokuwepo tungeweza kutumia muda mrefu zaidi.

 

“Tozo hizi ni kwa nia njema, tumekusanaya takribani bil 63 tangu tuanze zinazoweza kujenga vituo vya afya 150, vituo vingine 70 vinakuja ni matokeo ya hizi tozo. Serikali imeamua kuongeza kasi ya kuimarisha huduma kwa wananchi ndio maana inaitwa tozo ya mshikamano.

 

“Fedha hizi pia zimepelekwa maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kujenga na kumaliza maboma ya vyumba vya madarasa 560 kwa ajili ya wanafunzi wetu ambao wataanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwakani.

 

“Kumekuwa na maneno mbona huko nyuma hakukuwa na tozo na tulikuwa tunajenga, serikali imeamua kuongeza kasi ya kuimarisha huduma kwa wananchi ndiyo maana Waziri wa Fedha anaiita tozo ya mshikamano,tuweke hii tozo ili matatitizo yatatuliwe,” amesema Msigwa.

 

Leave A Reply