The House of Social Media
gunners X

Majaliwa: Wanafunzi Someni kwa Bidii

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watoto wa Kitanzania kujiwekea malengo na kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia taifa kupata maendeleo.

Amesema kuwa kwa upande wa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo hayo.

Amesema hayo leo Jumatatu, Januari 24, 2022 baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Gehandu na Nowu zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi, pia Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kuweka mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato ya halmashauri na iwapo itakapotokea Serikali imeweka mpango wa ujenzi wa mabweni watatumia fedha zao kama ujazilizi kwenye fedha hiyo.

Leave A Reply