The House of Social Media
gunners X

Rais Dk. Mwinyi Apokea Salamu Za Pole Kutoka Kwa CDF na Masauni

0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Machi 5, 2024 amepokea salamu za pole nyumbani kwake Ikulu Migombani kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali John Jacob Mkunda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni kufuatia kifo cha Baba Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassani Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29,  2024, Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2,  2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali John Jacob.

 

Leave A Reply