The House of Social Media
gunners X

Kundi D Laendelea Kutoa Upinzani Mkubwa, Simba Kupimana Ubavu na Stade Malien

0

Wababe wa Angola, Petro Atletico, wamelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Esperance de Tunis ya Tunisia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola.

Petro walikuwa wa kwanza kuona lango kupitia Tiago Reis dakika ya 49, lakini Esperance wakasawazisha dakika za lala salama kupitia Diakite dakika ya 89, na kulazimisha timu hizo kugawana pointi.

Matokeo hayo yanaifanya Petro Atletico kuendelea kusalia kinara wa Kundi D wakiwa na alama 4 baada ya michezo miwili, huku Esperance wakibaki nafasi ya pili wakiwa na alama 2 baada ya mechi mbili.

Stade Malien, ambao kesho wanawakaribisha Simba SC, wapo nafasi ya tatu na alama 1 baada ya mechi moja.
Simba SC wanaendelea kushika mkia bila alama yoyote kufuatia kipigo katika mchezo wao wa kwanza.

Matokeo ya Mechi

FT: Petro Atletico 🇦🇴 1–1 🇹🇳 Esperance Tunis
⚽ 49’ Tiago Reis
⚽ 89’ Diakite

FT: Power Dynamos 🇿🇲 0–1 🇪🇬 Pyramids
⚽ 51’ Reda

GENNO AFICHUA ALIVYOKOPWA na KIJANA wa DIAMOND na BABA LEVO – ”MSWAHILI – MUME WANGU ATAJUTA SANA”

Leave A Reply