The House of Social Media
gunners X

Hamisa Mobetto, Nana Doll na Queen Masanja Wampongeza Mama Chanja

0

Mrembo na mwanamitandao Hamisa Mobetto ameonesha kufurahishwa kwake na mafanikio yanayoendelea kupatikana na Mama Chanja, kufuatia kutimia kwa ndoto yake ya kumiliki gari.

Kupitia mitandao ya kijamii, Mama Chanja alithibitisha kupata gari lake jipya aina ya Subaru, akishiriki video akiwa pamoja na marafiki zake wakisherehekea hatua hiyo muhimu. Katika moja ya posti hizo, Hamisa Mobetto aliacha ujumbe wa pongezi uliovutia wengi, akisema:

“Nimekufurahia sana, hongera ❤️❤️”

Mbali na Hamisa, wasanii na watu maarufu wengine pia walijitokeza kumpongeza Mama Chanja, akiwemo Nana Dollz, Lamata, Tess, Queen Masanja pamoja na wengine, wakionesha furaha na kumuunga mkono katika mafanikio yake.

Ujumbe huo umeibua hisia chanya miongoni mwa mashabiki, wengi wakisifia mshikamano, upendo na kuhamasishana kati ya wanawake wanaofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na tasnia ya burudani kwa ujumla.

Leave A Reply