CAFCL: Yanga Wakamata Nafasi ya 3, Vita ya Kufuzu Kundi B Yapamba Moto

Mashindano ya TotalEnergies CAF Champions League yameendelea kushika kasi huku msimamo wa Kundi B ukiwa umebana vilivyo baada ya kumalizika kwa michezo ya raundi ya nne (Matchday 4), hali inayofanya kila mechi iliyosalia kuwa ya “kufa au kupona”.
Kwa mujibu wa takwimu za mashindano hayo, Al Ahly ya Misri bado wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 8, wakifuatiwa na Young Africans (Yanga) na AS FAR Rabat wenye alama 5 kila mmoja, huku JS Kabylie wakiburuza mkia kwa alama 2.
Matokeo hayo yanaiweka Yanga katika nafasi ya tatu, lakini tofauti ya pointi ni ndogo sana kiasi kwamba nafasi mbili za juu bado ziko wazi kwa timu zote tatu za juu.


