Rais Samia Arejea Kutoka Mkutano wa Dunia wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), tarehe 6 Februari 2026.
Rais alikuwa nchini humo kushiriki Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS 2026) pamoja na Uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji Afrika (Global Africa Investment Summit – GAIS), mikutano inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, ubunifu wa kiutawala na kuvutia uwekezaji barani Afrika.
Ushiriki wake katika majukwaa hayo unatajwa kuwa sehemu ya jitihada za Tanzania kuimarisha diplomasia ya uchumi na kufungua fursa mpya za uwekezaji na maendeleo ya taifa.

HOTUBA NZITO ya WAZIRI MKUU MWIGULU AKIAHIRISHA BUNGE – ATOA MALENGO na MIKAKATI ya SERIKALI

