The House of Social Media
gunners X

Serikali Yatoa Bilioni 200 Kuwezesha Vijana na Wanawake Kiuchumi

0
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka, hundi ya shilingi bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mitaji ya kuwawezesha vijana na wanawake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Februari 05, 2026. kulia ni kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) William Lukuvi.

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, hundi ya shilingi bilioni 200 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwezesha vijana na wanawake mitaji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Makabidhiano hayo yamefanyika Februari 05, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, yakilenga kuongeza fursa za ajira, ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi kwa makundi hayo muhimu katika jamii.

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar hundi ya shilingi bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mitaji ya kuwawezesha vijana na wanawake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Februari 05, 2026.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Nchemba alisema fedha hizo zitasaidia kukuza biashara ndogo na za kati pamoja na miradi ya ubunifu itakayochochea maendeleo ya taifa.

Katika hafla hiyo, kulia kwa Waziri Mkuu alikuwepo Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, huku kushoto akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha uchumi jumuishi unaowapa nafasi vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi.

Leave A Reply