
Ferrari imevunja utulivu wa wapenzi wa magari na tech baada ya kutangaza rasmi jina la gari lake la kwanza la umeme, lililokuwa likijulikana kwa jina la muda la “Elettrica.” Jina rasmi ni Luce (inavyotamkwa “LOO-chay”), neno la Kiitaliano lenye maana ya “mwanga.”

Katika tukio lililofanyika kwenye TransAmerica Pyramid, San Francisco, Rais wa Bodi ya Ferrari, John Elkann, alisema kuwa kumuita gari hili tu “electric Ferrari” kungepunguza uzito wa ubunifu na mradi wa kipekee uliokuwa ukifanywa kwa kizazi kimoja.
“Luce inakupa hisia za siku za usoni, hisia ya mwanga, kasi, ubunifu na mambo mengine mengi yaliyowezesha kuunda mradi huu wa ajabu,” alisema Elkann.




