The House of Social Media
gunners X

Meridianbet Yatoa Fimbo za Kutembelea kwa Watu Wasioona Dar

0

Meridianbet Tanzania imeandika historia nyingine ya uwajibikaji kwa jamii kwa kukabidhi msaada wa fimbo za kutembelea kwa watu wenye ulemavu wa kuona jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Tanzania Association of the Blind (T.A.B) yaliyopo Kinondoni, ikilenga kuimarisha ustawi na uhuru wa watu wasioona katika shughuli zao za kila siku.

Tukio hilo lilihudhuriwa na Mwenyekiti wa T.A.B pamoja na wanachama wa chama hicho, huku upande wa Meridianbet ukiwakilishwa na timu yake iliyoongozwa na Afisa Uhusiano wa Umma, Nancy Ingram. Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa Meridianbet alieleza kuwa msaada huo unatokana na imani ya kampuni katika kurudisha kwa jamii na kusaidia makundi yenye mahitaji maalum kama sehemu ya misingi na maadili yake ya uendeshaji.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa T.A.B aliipongeza Meridianbet kwa kugusa maisha ya watu wasioona kupitia msaada huo muhimu. Alisema fimbo hizo zitachangia kuongeza usalama, kujiamini na uhuru wa kutembea kwa wanachama wao, na kwamba ushirikiano kama huo ni nguzo muhimu katika kujenga jamii inayojali na kuthamini watu wenye ulemavu.

Meridianbet imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii nchini, ikiwa ni pamoja na kusaidia makundi yenye uhitaji kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya na endelevu. Kupitia mpango huu wa CSR, kampuni inaonesha kuwa mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na wajibu wa kuchangia maendeleo ya jamii inayoiwezesha kufanya kazi.

Msaada huo wa fimbo za kutembelea ni ishara ya mshikamano na uwajibikaji wa Meridianbet kwa jamii ya Watanzania. Kampuni hiyo imeahidi kuendeleza juhudi zake za kusaidia watu wenye ulemavu na kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha kila kundi katika jamii linapata fursa na msaada stahiki kwa maendeleo yao.

Leave A Reply