The House of Favourite Newspapers

Tamsha la Fiesta Kufanyika Dar Mwezi Huu

MKURUGENZI Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga, kupitia kipindi cha Clouds 360 leo,  amedhibitisha taarifa  za kurudiwa kwa tamasha la Tigo Fiesta kabla ya mwaka huu kwisha.

Kusaga ameyasema hayo wakati wa kuadhimisha mwaka wa 19  tangu kuanzishwa kwa Clouds Media Group.

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga.

Tamasha la Fiesta jijini Dar es Salaam lilitakiwa kufanyika Novemba 24, 2018 lakini halikufanyika na sababu ya msingi haikutajwa zaidi ya viongozi kusema kuwa tatizo hilo lilikuwa nje ya uwezo wao.

Alichokisema Joseph Kusaga:

“TIGO FIESTA 2018 lazima ifanyike kabla mwaka kuisha, nimezungumza hadi na Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwamba pengine suala ni venue,  hili jambo limepenyezwa kwa viongozi wa serikali tumekaa tumezungumza.”

 

Comments are closed.