EWURA Yatangaza Bei Mpya za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa kuanzia leo
Dar es Salaam, Januari 7, 2026 – Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo mpya za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoanza kutumika nchini kuanzia leo Jumatano, zikionesha mabadiliko mbalimbali kulingana na bandari na aina ya bidhaa.


