The House of Favourite Newspapers

Inasikitisha… Watoto Wafunguka Walivyoingizwa Kwenye Matumizi ya ‘Unga’

Mihayo Msikhela akizungumza.

 

 

Nuru Saleh, mmoja wa waathirika wa madawa ya kulevya aliyeacha.

Mtoto Yusra akitoa ushuhuda wake.

Mhe. Makonda akiwa na watoto Zuhura na Yusra

Kutoka kushoto ni mtoto aliyekuwa amejiingiza katika madawa ya kulevya, Zuhura Othman, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na mtumiaji aliyeacha madawa, Nuru Saleh.

Watoto hao wakiwa wamekaa na watu wengine.

Dunia katili! Wasichana wawili wadogo, Zuhura Othman (16) na Yusra Abdallah ni miongoni mwa waathirika wa madawa, ambao wamekiri mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, waandishi wa habari na wadau mbalimbali waliokutana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam.

Wasichana hao wadogo, wameeleza kwamba kwa kipindi kirefu, walikuwa watumiaji wa madawa hayo, huku wakijiingiza kwenye vitendo vingine hatari, ikiwemo kufanya biashara hatari ya kuuza miili yao ambapo mmoja kati yao, ni mwathirika wa Virusi vya Ukimwi.

Wasichana hao wanaolelewa katika Kituo cha Soba House, Kigamboni jijini Dar es Salaam wametoa simulizi iliyogusa hisia za watu wengi waliohudhuria kwenye mkutano huo ambapo… alisema alianza kutumia madawa ya kulevya akiwa na umri wa miaka 9, na kwamba alishawishiwa kuingia kwenye matumizi hayo na mwanaume aliyekuwa mpenzi wake, ambaye kwa sasa amefariki dunia kwa Virusi vya Ukimwi.

PICHA ZOTE NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS.

Comments are closed.