The House of Favourite Newspapers
gunners X

SHORT FILM: Kwa Mapenzi Haya, Unaweza Kufa! Tazama Video Hii

FILAMU fupi ya mapenzi yenye ubora wa kimataifa iitwayo Kinje In America, iliyorekodiwa nchini Marekani na msanii wa filamu za Kibongo, Chris Lubango a.k.a Kinje akishirikiana na mwanadada anayefanya poa kwenye filamu za Marekani, Pendo Jones ‘Babelanta’ imetua nchini na kwa mara ya kwanza na imeoneshwa leo kupitia Global TV.

Katika filamu hiyo, Kinje anafunga safari mpaka nchini Marekani kumfuata mpenzi wake, Babelanta lakini baada ya kufika huko, alichokitegemea sicho alichokutana nacho. Huo unakuwa mwanzo wa kisa cha kusisimua cha mapenzi, kilichosheheni matukio ya kuhuzunisha na kuumiza moyo.

 

“Ni bonge la filamu, baada ya kusota kwa muda mrefu hapa Bongo, nimepata bahati ya kwenda Marekani na kujionea wenzetu wanavyofanya kazi zao. Nimefika Hollywood na kiukweli, sisi hapa nyumbani bado sana katika filamu.

“Nikiwa huko nikaona si vyema nirudi mikono mitupu, nikakaa chini na mwenzangu Babelanta ambaye makazi yake ni Houston Texas, huyu ni Mbongo lakini anaishi kule na ni mdau mkubwa wa filamu, tukawaandalia zawadi Watanzania na zawadi yenyewe ndiyo hii, Kinje in America.

 

“Sitaki kusema sana kuhusu ubora wake kwa sababu kila mtu atajionea mwenyewe, nawashauri wasanii, wadau wa filamu na mashabiki, waitazame Kinje in America wajionee tofauti,” alisema Kinje.

Naye Babelanta, ameliambia Mikito Nusu Nusu, kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akiwafuatilia wasanii wa kike wenye majina makubwa Bongo kama Irene Uwoya, Wema Sepetu, Kajala Masanja na wengineo, lakini haridhishwi na uwezo wanaouonesha kwenye filamu, ndiyo maana ameamua kuingia ‘mazima’ kuwaonesha tofauti.

Fuatilia Filamu hiyo Global TV hapa

Comments are closed.