The House of Favourite Newspapers

BATA LA YOUNG DEE MAREKENI KWELI…BONGO BAHATI MBAYA

Maisha ndo’ hayahaya,

so n’taenda wapi,

Bongo bahati mbaya,

Hollywood yetu Masaki,

Usishangae natamba,

Halafu we’ hauna chambi,

mi mwembamba ila napiga show

za kitambi….

Tupo Bongo bahati mbaya tu,

Karibu Ulaya…

NI mion-goni tu mwa mistari inayo-patikana katika Ngoma ya Bongo Bahati Mbaya (BBM) ya David Genz ‘Young Dee’ aliyoitoa miaka miwili iliyopita na kugeuka ngoma ya taifa. 

 

Katika ngoma hii, Young Dee alitaka kuonesha jamii kuwa tusikatae vya kwetu! Wote wanaokimbilia ‘mbele’ Ulaya huko kuna vitu sawa na Bongo tu. Akafananisha baadhi ya mazingira ya Marekani yalivyo sawa na Bongo tu! Kwa sasa Young Dee ni kama amepindua sarafu chini ya maji! Amevuka boda na kutinga katika nchi ya Trump, Marekani na siyo kutinga tu, anakula bata si la kitoto!

Shoo zake Tangu ametinga katika nchi hiyo na kuweka makazi pande za Baltimore, Maryland, Young Dee amekuwa akipata shoo kubwa mbalimbali.

 

Ameshafanya shoo iliyotambulika kama Afro Vibez katika Ukumbi wa Golf Ultra Lounge pande za Georgia, Marekani. Shoo nyingine ni Empire Thursdays ndani ya Empire Lounge, Washington DC, Marekani, Supreme Sunday ndani ya Dirty Martin, Washington DC, African Caribbean ndani ya Club Elevant, Washington DC, Lit Party ndani ya Mix Lounge, Georgia.

BATA LAKE SASA

Amekuwa akionekana katika picha na mandinga ya hatari kama siyo anaendesha bali yupo nalo pembeni. Miongoni mwa magari hayo ni Mercedes Benz C-Class, Lamborghini Aventador na mengine ya maana. Pia amekuwa akionesha maburunguru ya Dola za Kimarekani ambazo kwa hesabu za harakaharaka Kibongobongo zinaweza kufikia hadi shilingi milioni 100.

AKUTANA NA MASTAA

Kubwa kuliko yote, mbali na kupiga shoo katika kumbi mbalimbali, Young Dee amepata pia fursa ya kukutana na wakali katika muziki duniani ambao wanaishi Marekani.

 

Alianza kukutana na Rapa Howard Bailey Jr ‘Chingy’ aliyewahi kubamba na ngoma kibao kama Right Thurr na Balla Baby. Pia alikutana na staa mwingine wa R&B, Mario Dewar Barrett ‘Mario’ ambaye naye aliwahi kutikisa na ngoma kibao kama Let Me Love You na Just A Friend. Wapo wakali wengine aliokutana nao kutoka Afrika wanaotikisa Marekani kama King Jollof ‘Indo Baba’ anayetikisa na Ngoma ya Sho Le na Berejo akiwa na asili ya Nigeria.

ALIPOTOKA

Young Dee alianza kukubalika alipokuwa na umri wa miaka 16 baada ya kutoa ngoma yake ya kwanza ya Teacher ambayo ilimtambulisha vyema na kumfanya miongoni mwa wakali waliokuwa na umri mdogo akiwa sambamba na Dogo Janja. Baada ya hapo alionesha makali yake kwa kutoa ngoma kali ambazo ni Dada Anaolewa, Furaha, Hands Up, Utani, Gari Yangu, Noma Kweli na nyingine nyingi.

Comments are closed.