The House of Social Media
gunners X

Balama Mambo Safi Sauz

0

MAMBO yanaelekea kuwa poa kwa kiungo wa Yanga, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ kufuatia kufanyiwa upasuaji wa goti lililokuwa likimsumbua kwa muda.

 

Mapinduzi alipelekwa Afrika Kusini hivi karibuni kupatiwa matibabu kutokana na kuvunjika mguu tangu msimu uliopita.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, tayari kiungo huyo anaendelea vyema na matibabu na wiki ijayo akitarajiwa kurudi hapa nchini.“

 

Mapinduzi anaendelea vizuri, tumewasiliana na madakari wake wamesema anaendelea vyema na tayari ameshafanyiwa upasuaji, wiki ijayo anatarajia kurejea nchini,” alisema Mwakalebela.

STORI: KHADIJA MNGWAI, DAR

Leave A Reply