The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kambole Asema Anakuja Yanga, Ataja Makubaliano ya Mkataba Wake

0
Lazarous Kambole amemaliza Mkataba wake na Kaizer Chiefs

 

MSHAMBULIAJI raia wa Zambia, Lazarous Kambole, amefichua kuwa, suala lake la kujiunga na Yanga lipo chini ya wakala wake, lakini muda si mrefu atakuwa mchezaji wa timu hiyo.

 

Mzambia huyo anatajwa kumalizana na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kaizer Chief ya Afrika Kusini ambapo amemaliza mkataba wake.

 

Ikumbukwe hii siyo mara ya kwanza kwa Yanga kumtaka mshambuliaji huyo ambapo msimu uliopita walishindwa kufikia muafaka kutokana na dau lake la usajili kuwa kubwa hali iliyofanya Yanga kukaa pembeni kabla ya kumrejea tena mwaka huu.

Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka kwao Zambia, Kambole alisema kila kitu kipo sawa, hivyo ni jambo la muda yeye kutua Yanga.

Kambole ataja kurudi Yanga SC

“Hapa tunavyozungumza nimekuja hospitali kumleta mtu, lakini kitu ambacho naweza kukwambia kwa sasa mambo yote yanakwenda sawa maana wakala ndiyo yupo katika kushughulikia vitu vya mwisho, hivyo ni jambo la kusubiria.

 

“Siwezi kusema ni kwa muda gani wamekubaliana huo mkataba, niache kwa sasa halafu nitarejea kwako kukueleza kila kitu, lakini nakuja Yanga,” alisema Kambole huku akionekana mwenye furaha.

STORI NA IBRAHIM MUSSA

BAJETI KUU – DENI LA TAIFA LAONGEZEKA, SERIKALI YAFUTA ADA FORM 5 na 6, MWIGULU ANAWASILISHA

Leave A Reply