The House of Favourite Newspapers
gunners X

Babu Tale Kuwalipia Tiketi za Ndege Wasanii Waliotajwa Tuzo za Afrimma

0
Babu Tale

MBUNGE wa Morogoro Mashariki na Meneja wa Wasanii wa muziki chini ya lebo ya WCB, Hamisi Taletale ameainisha dhamira yake ya kupambania tiketi za kuwafikisha Marekani wasanii saba wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu kwa lengo la kuleta matokeo chanya kwenye ukuaji wa muziki na Tasnia kwa ujumla.

 

Tale pia ameliomba Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kushughulikia upande wa VISA kwa Wasanii hao kwani tayari wana barua za mialiko kushiriki katika hafla ya utoaji wa Tuzo hizo.

 

Tale ameandika; “Kwa sasa Muziki wetu umekua na kuifikia Dunia, ndio maana Wasanii wetu wameendelea kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali kubwa ikiwepo hizi tuzo za AFIMMA @afrimma.

 

Tuzo hizi zitafanyika nchini Marekani mwaka huu 2022. Kwa kutambua umuhimu wa kuwakilisha nchi yetu, uwepo wangu kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu na dhima ya kukuza sanaa yetu, nadhamiria kuhangaikia tiketi Saba za Wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizi. NB: Hatakaewahi kupata VISA ndiye atakaewahi kupata ticket.

Mbunge wa Morogoro Mashariki Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale

Hivyo niombe Baraza la Sanaa Tanzania @basata.tanzania (BASATA), kusaidia upatikanaji wa VISA za Wasanii waliochaguliwa kwani wote wanabarua za mwaliko.

 

Tuzo hizi ni muhimu kwa ukuaji wa muziki wetu na kulitangaza Taifa letu kwenye kile alichokianzisha Mheshimiwa Rais wetu cha kuvuta watalii nchini. Hii ikawe sehemu ya kila msanii shiriki kuizungumzia Royal tour akiwa huko nchini Marekani”

Leave A Reply