The House of Favourite Newspapers
gunners X

Serikali Yaendelea Kurahisisha Utoaji Wa Hati za Viwanja Kwa Njia Ya Kidijitali

0
Kamishina wa Ardhi msaidizi Kanda ya Dar es salaam akikabidhi hati ya kiwanja kwa wananchi katika zoezi liliambana Clinic ya Ardhi kutoka Kwa maafisa Ardhi wa Wizara na Manispaa ya Ilala kwenye viwanja vya shule ya msingi Segerea

 

Kamishina wa Ardhi Msaidizi mkoa Dar es salaam Bw. Idrisa Kayera ameshiriki Clinic ya Ardhi Segerea na kutoa hati 229 za viwanja Kwa wananchi mbalimbali katika viwanja vya shule ya msingi Segerea wilaya ya ilala jijini Dar es salaam.

 

Akizungumza baada ya zoezi hilo Bw. Kayera amesema upatikanaji wa hati za viwanja umekua rahisi zaidi na unafanyika kidijitali ambapo mwananchi anaweza kulipia gharama za hati Kwa njia ya simu na kuipata hati yake muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu zote zinazohitajika,

Mratibu wa Urasimishaji mkoa Dar es salaam , Laurent Mswani akikabidhi hati ya kiwanja mkazi wa segerea kwenye zoezi la ugawaji hati lililoambana na clinic za elimu ya Ardhi kutoka Kwa maafisa Ardhi kutoka Wizarani na halimashauri ya Ilala

 

Kamishina Kayera ambaye aliambana na maafisa Ardhi na wataalamu mbalimbali wa masuala ya Ardhi kutoka Wizarani na Manispaa ya Ilala, amesisitiza kuwa zoezi la ugawaji hati kwasasa linaambana na utoaji elimu ya umilikishwaji Ardhi, utatuaji wa migogoro, elimu ya Mipango miji pamoja na namna ya kulipa Kodi baada ya umilikishwaji kukamilika.

Kwa upande wake Afisa Ardhi mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Bi. Helen Philip ameongeza kuwa serikali inachukua hatua sitahiki kuhakikisha changamoto zitokanazo na umilikishwaji Ardhi Kwa wananchi zinapungua kupitia clinic za elimu zinazotolewa maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na nchi nzima Kwa ujumla.

Afisa Ardhi mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Helen Philip akikabidhi hati Diwani kata ya Segerea baada ya kukamilisha taratibu zote za Urasimishaji kwenye kiwanja chake

 

Ebenezer Kwayu ni miongoni mwa wakazi wa segerea ambaye amelipia gharama za umilikishwaji wa kiwanja kupitia simu yake na kukabidhiwa hati yake baada ya muda mfupi amewatoa hofu wananchi wengine na kuwahamasisha kufatilia hati zao ili kuepuka migogoro ya mipaka ambayo imekua ikiripotiwa mara Kwa mara katika maeneo mbalimbali.

 

Zoezi hilo la ugawaji hati litaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kupitia ofisi ya Kamishina msaidizi wa Ardhi Kanda ya Dar es salaam.

 

Leave A Reply