The House of Favourite Newspapers
gunners X

Viongozi Waliopinduliwa Madarakani Tangu 2011 Nchi za Kiarabu

0
Bashar al-Assad

Bashar al-Assad ameingia kwenye orodha ya viongozi mashuhuri wa nchi za Kiarabu waliopinduliwa tangu kuanza kwa maandamano katika nchi za kiarabu, Zine al-Abidine Ben Ali (Tunisia, 2011) ni miongoni mwa Viongozi waliopinduliwa baada ya dhoruba ya mapinduzi ya kiraia nchini Tunisia pamoja na serikali yake, Ikumbukwe kuwa Zine al-Abidine Ben Ali, aliitawala Tunisia kwa miaka 23

Kiongozi mwingine ni Hosni Mubarak (Misri, 2011 aliitawala Misri kwa miaka 30 kabla ya maasi ya nchi za Kiarabu. Mabadiliko ya serikali nchini Tunisia yalichochea kuondolewa Mubarak nchini Misri, Mubarak alijiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali yake, yaliyoanza Januari 25 katika uwanja wa Tahrir mjini Al Khahira.

Ali Abdullah Saleh

Ali Abdullah Saleh (Yemen, 2011) Baada ya miezi kadhaa ya maandamano yaliyopindua serikali za nchi za Kiarabu, dhoruba hiyo ilifika Yemen, ambapo baada ya miezi kadhaa ya upinzani kati ya wananchi na serikali, Rais Ali Abdullah Sale alikubali kung’atuka madarakani mnamo Novemba 23, 2011, baada ya kupona majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio la bomu kwenye ikulu yake.

Muammar Gaddafi

Muammar Gaddafi (Libya, 2011) Wimbi hilo la mabadiliko lilifikia Libya ambapo liliipindua serikali ya kiongozi wake aliyekaa madarakani kwa muda wa miaka 42. Muammar Gaddafi alikuwa kiongozi wa kwanza kuuawa baada ya wimbi la kupinduliwa kwa tawala katika nchi za Kiarabu. Ikumbukwe kuwa Muammar Gaddafi aliingia madarakani Septemba 1969 baada ya mapinduzi ya ghafla, na kumuangusha mfalme Idris anayeungwa mkono na Uingereza.

Bashar al-Assad (Syria, 2024) Rais wa hivi karibuni zaidi ambaye serikali yake ni Bashar al-Assad, baada ya kundi la waasi kuongoza maasi dhidi ya serikali yake Jumapili, Desemba 8, 2024. Familia ya Assad imeitawala Syria kwa miaka 53.

Rais Bashar al-Assad alichukua madaraka mwaka 2000, baada ya babake kutawala kwa miaka 30.
Lakini wiki iliyopita, kundi la Kiislamu, Hayat Tahrir al-Sham (HTS) lilifanikiwa kufanya mashambulizi mabaya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, baada ya kushirikiana na makundi mengine ya waasi.

Waasi hao waliuteka mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria, Aleppo, na kuelekea kusini hadi mji mkuu, Damascus, ambako walizidi nguvu jeshi la Syria.
Urusi baadaye ilitangaza kuwa Assad na familia yake wamepewa hifadhi ya kisiasa huko Moscow.

MC PILIPILI AINGILIA KATI UGOMVI wa MARTHA MWAIPAJA na NDUGU YAKE – “MUNGU ANASIMAMA na NINYI”…

Leave A Reply