The House of Favourite Newspapers

Pamba Jiji Yatajwa Kukwamisha Ratiba ya Mazoezi Uwanja Mkapa

0

Baada ya taarifa kusambaa mitandaoni ikionesha wachezaji wa Pamba Jiji wakifanya mazoezi gizani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Serikali imesema timu hiyo ilifika uwanjani hapo pasipo kutoa taarifa rasmi ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga SC Septemba 24, 2025.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa wakati timu hiyo imewasili uwanjani hapo saa 12:35 jioni, wataalamu wa umeme walikuwa wamekwisha ondoka na hivyo ikawalazimu kuwarudisha kazini na kufanikiwa kuwasha taa za uwanja huo saa 1:8 usiku.

“Wizara imesikitishwa na usambazaji wa picha jongefu zinazoonesha wachezaji wakifanya mazoezi gizani licha ya kuwa chanzo chake ni makosa ya timu ya Pamba Jiji FC yenyewe, na imekiona kitendo hicho kama ni kuharibu heshima na taswira ya menejimenti ya uwanja, ambayo imekuwa ikifanya kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa,” imesema taarifa iliyotolewa na wizara.

Leave A Reply