Israel Yamkamata Mjukuu Wa Mandela, Ramaphosa Atoa Mwito Wa Kuachiliwa Mara Moja

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameitaka Israel kuwaachia mara moja wanaharakati wa Afrika Kusini waliokamatwa na jeshi la majini la Israel baada ya kuizuia “Global Sumud Flotilla”, msafara wa meli uliokuwa ukielekea Gaza kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.
Kati ya waliokamatwa ni pamoja na mjukuu wa Nelson Mandela, Nkosi Zwelivelile “Mandla” Mandela, huku taarifa zikithibitisha uwepo wa raia wengine wa Afrika Kusini.
Ramaphosa ameeleza kitendo hicho kama “utekaji” na kulaani hatua ya Israel akisema ni “tukio jingine kubwa la kudhalilisha mshikamano wa kimataifa na Gaza.”
Boti moja, Mikeno, iliripotiwa kufanikisha kuvuka na kuingia maji ya Palestina, lakini mawasiliano nayo yamepotea.