The House of Favourite Newspapers

Sengerema Yazizima Kijani! Wananchi Wamiminika Kumsikiliza Dkt. Samia

0

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya mnadani wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, kumlaki na kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakazi wa Sengerema walijitokeza mapema asubuhi wakiwa wamevalia mavazi ya kijani na njano, wakiwa na mabango yenye jumbe za kumuunga mkono Dkt. Samia, huku nyimbo za kampeni na nderemo zikisikika kila upande.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na vyombo vya habari walisema kuwa kura zao tayari ni za Dkt. Samia, wakisisitiza kuwa wanataka kuona uendelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imeanza chini ya uongozi wake.

“Mgombea Urais tutakayempa kura za ndiyo na za kishindo ni Samia. Kama jina hilo halikuhusu, basi pita kuleee… hapo tumeelewana!” alisema mmoja wa wananchi kwa shangwe kubwa.

Ziara ya Dkt. Samia mkoani Mwanza ni sehemu ya kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinazolenga kuimarisha uelewa wa wananchi juu ya ilani ya chama na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi kijacho.

Leave A Reply