Zubeir Ali Maulid Achaguliwa Tena Kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Zanzibar, Novemba 6, 2025 — Zubeir Ali Maulid amechaguliwa tena kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa kipindi cha tatu mfululizo, katika kikao cha kwanza cha Baraza la 11 la Wawakilishi kilichofanyika leo Alhamisi.
Zubeir, ambaye anatoka Chama cha Mapinduzi (CCM), alipata kura 53 sawa na asilimia 94.6 ya kura zote halali, na kuwabwaga wapinzani wake watatu.

