Live: Rais Dkt. Samia Akitunuku Kamisheni Kwa Maafisa Wanafunzi Wa Jwtz, Monduli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anongoza hafla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka makundi mawili ya mafunzo: kundi la 06/22 – BMS na kundi la 72/24 – Regular. Hafla hiyo imefanyika tarehe 22 Novemba 2025, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (Tanzania Military Academy – TMA) Monduli, mkoani Arusha.
Katika tukio hilo muhimu la kijeshi, Rais Samia atawapandisha vyeo maafisa wanafunzi na kuwatunuku Kamisheni kama ishara ya kuhitimu mafunzo yao rasmi ya kijeshi, hatua inayowatambulisha kama maafisa kamili wa JWTZ. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, makamanda wa JWTZ, familia za wahitimu, pamoja na wageni waalikwa.


