Polisi Mkoa wa Mbeya Wakamata Mwandambo Akidaiwa Kusambaza Maneno ya Uchochezi Mitandaoni

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limemkamata mwalimu wa shule ya awali Saint Clemence, Clemence Kenani Mwandambo, kwa tuhuma za kusambaza maneno ya uchochezi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi ya Kamanda wa Polisi, mtuhumuwa alikamatwa tarehe 21 Novemba 2025 saa 5:20 asubuhi katika eneo la Uzunquni “A”, Jiji la Mbeya, mara baada ya polisi kupokea taarifa kwamba alikuwa akituma na kusambaza ujumbe wenye ubishani na uchochezi kupitia akaunti zake za Facebook na Instagram.


