The House of Favourite Newspapers
gunners X

Msando: Serikali Haina Ajenda ya Siri Dhidi ya Askofu Gwajima – Video

0
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando.

Serikali imesisitiza kuwa hakuna mtego wala mpango wowote wa kumkamata Askofu Dkt. Josephat Gwajima kufuatia hatua ya kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima analoliongoza.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, alipofika katika Kanisa hilo leo Jumanne, Novemba 25, 2025. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, alilolitoa Novemba 24 akilitaka Kanisa kufunguliwa ili waumini waweze kuendelea na ibada chini ya uangalizi maalum.

Wakili Msando alitoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa zilizoenea mitandaoni zikidai kuwa kufunguliwa kwa Kanisa hilo kunaweza kuwa ni mtego wa kumkamata Askofu Gwajima. Alisisitiza kuwa serikali haina ajenda ya siri na kwamba lengo kuu ni kuhakikisha ibada zinaendelea kwa utulivu.

Aidha, amewaagiza viongozi wa Kanisa hilo kufanya ukaguzi na ulinganifu wa kila kilichofanyika tangu walipofunga Kanisa hadi kufunguliwa kwake. Ameeleza kuwa endapo wataona dosari yoyote hawapaswi kusita kuwasilisha taarifa ofisini kwake.

Leave A Reply