Al Ahly Yaingia Vitani Kumsajili Fiston Mayele, Yapanga Kumlipa Sh180 Mil kwa Mwezi

Klabu ya Al Ahly Cairo ya Misri imeingia rasmi kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji hatari wa Pyramids FC, Fiston Mayele, katika dirisha dogo la usajili la Januari mwakani.
Taarifa kutoka Misri zinaeleza kuwa miamba hiyo ya Afrika imeonyesha dhamira ya dhati ya kumvuta nyota huyo kwa kutenga mshahara mnono wa Paundi za Misri 3,476,902 (sawa na takribani Sh180 milioni za Tanzania kwa mwezi), kifurushi ambacho kinaaminiwa kuwa sehemu ya mpango wa Al Ahly kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea michuano ya ndani na kimataifa.
Mayele, ambaye msimu uliopita aliibuka Mchezaji Bora wa Vilabu vya Afrika (CAF), ameendelea kung’ara akiwa katika msimu wake wa kwanza na Pyramids FC. Alijiunga na mabingwa hao wa fedha kutoka Misri akitokea Yanga SC kwenye msimu wa 2024/25, baada ya kuiongoza klabu hiyo ya Tanzania kwenye mafanikio makubwa katika ligi na mashindano ya CAF.
Katika kipindi chake Pyramids, Mayele ameendelea kuthibitisha ubora wake kwa kasi ya kutengeneza na kufunga mabao, jambo ambalo limezivutia klabu kadhaa kubwa barani Afrika, huku Al Ahly ikionekana kuweka mezani dau linaloweza kuikatia ushindani timu yoyote.
STORI NA WIRBERT MOLAND | GPL


