Bernabéu Yawaka Moto! Real Madrid Yapoteza Tena, Xabi Aingia Hatarini

Kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, yupo kwenye wakati mgumu zaidi tangu achukue timu hiyo, baada ya kurekodi kipigo cha pili mfululizo. Usiku wa jana Madrid walipoteza 2-1 dhidi ya Manchester City katika dimba la Santiago Bernabéu, siku chache tu baada ya kulala 2-0 mbele ya Celta Vigo kwenye La Liga.
Kipigo hicho kimetikisa mazingira ndani ya Madrid, huku mashabiki na wachambuzi wakianza kuhoji mwenendo wa timu na mbinu za Alonso, wakidai kikosi hicho “hakionyeshi meno” katika mechi kubwa.
MATOKEO MENGINE YA USIKU
Haya ndiyo matokeo kamili kutoka viwanja mbalimbali barani Ulaya:
Club Brugge 0-3 Arsenal
⚽ 25’ Madueke
⚽ 47’ Madueke
⚽ 56’ Martinelli
Arsenal waliutawala mchezo na kupata ushindi mnono ugenini kupitia ubora wa Madueke na kasi ya Martinelli.
Athletic Bilbao 0-0 PSG
Mchezo ulimalizika bila mabao licha ya juhudi za timu zote mbili kutafuta ushindi.
Bayer Leverkusen 2-2 Newcastle
Mchezo mkali uliomalizika kwa sare ya mabao manne, kila timu ikionesha ubora wa safu za ushambuliaji.
Benfica 2-0 Napoli
Benfica walipata pointi muhimu nyumbani kwa kutumia vyema mapungufu ya Napoli.
Juventus 2-0 Pafos
Juve waliendelea na mwenendo mzuri kwa kupata ushindi rahisi mbele ya mashabiki wao.
Dortmund 2-2 Bodo/Glimt
Sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo uliokuwa na kasi na ubadilishanaji mwingi wa mashambulizi.

